Mchanaji maarufu kutoka Zanzibar ambae ana style yake ya kipekee ya uchanaji anayoiita Taarap, amezungumza kwenye interview na Ayo TV. Rapper huyo amesema kuwa medias zitoe airtime kubwa kwa wasanii wanaofanya mziki ndani ya nchi maana nje hawapati airtime, kwahiyo wanakosa nafasi kusikika kote ndani na nje. Ambapo kwa wenzetu imekuwa ni tofauti ambapo wao wanaupa mziki wao airtime kubwa kuliko mziki wa nje, na pengine hawatoi kabisa airtime kwa miziki ya nje. Amesema hayo baada ya kupata nafasi ya kushiriki katika Tamasha la muziki huko Afrika Kusini na kuona nyimbo za mataifa mengine kutosikilizwa
0 Comments